Mwenyekiti wa Kamati ya kupigania kufunguliwa kwa gazeti la
Mwanahalisi Marcossy Albanie(kulia) akisisitiza jambo katika mkutano huo na
kusema kama itashindikana kufanya hivyo wataitisha maandamano ya kupinga hatua
ya serikali kufungia gazeti hilo na kunyima haki za binadamu. Katikati ni
Mwenyekiti wa MISA –TAN Mohammed Tibanyendera na kushoto ni Afisa Habari wa Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu Bw. Elias Mhegera.
Agosti 21, 2012
Watetezi wa haki za binadamu na asasi nyingine za kiraia
zimerejea wito wao wa kuitaka serikali kulifungulia mara moja bila masharti
gazeti la Mwanahalisi ambalo limekuwa kipenzi cha Wananchi.
Wameisihi Serikali kutekeleza hilo kwa kuangalia maslahi
mapana ya jamii badala ya kuangalia maslahi ya baadhi ya viongozi wenye maslahi
fulani katika kutimiza malengo binafsi.
Wamesema pamoja na mambo mengine, hawakubaliani na Kauli ya
Waziri Mkuu na wengine walioitaka Mwanahalisi waende mahakamani kutafuta haki
yao kwa kuwa serikali yenyewe haikutumia njia ya mahakama katika kulifungia
kazeti.
Tuwasiliane: mhegera@gmail.com
0754-826272

watekaji wa Dr Stephen Ulimboka hawafahamiki walipo, mauaji ya Daud Mwangosi, usanii mtupu, mashambulizi dhidi ya Absalom Kibanda ah shauri zake, je uslama wetu upo wapi? je tutafika?
JibuFuta