Jumapili, 6 Julai 2014

FUNGULIA MWANAHALISI FUNGA MAFISADI




Mwenyekiti wa Kamati ya kupigania kufunguliwa kwa gazeti la Mwanahalisi Marcossy Albanie(kulia) akisisitiza jambo katika mkutano huo na kusema kama itashindikana kufanya hivyo wataitisha maandamano ya kupinga hatua ya serikali kufungia gazeti hilo na kunyima haki za binadamu. Katikati ni Mwenyekiti wa MISA –TAN Mohammed Tibanyendera na kushoto ni Afisa Habari wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Bw. Elias Mhegera.
  Agosti 21, 2012
Watetezi wa haki za binadamu na asasi nyingine za kiraia zimerejea wito wao wa kuitaka serikali kulifungulia mara moja bila masharti gazeti la Mwanahalisi ambalo limekuwa kipenzi cha Wananchi.
Wameisihi Serikali kutekeleza hilo kwa kuangalia maslahi mapana ya jamii badala ya kuangalia maslahi ya baadhi ya viongozi wenye maslahi fulani katika kutimiza malengo binafsi.
Wamesema pamoja na mambo mengine, hawakubaliani na Kauli ya Waziri Mkuu na wengine walioitaka Mwanahalisi waende mahakamani kutafuta haki yao kwa kuwa serikali yenyewe haikutumia njia ya mahakama katika kulifungia kazeti.
Tuwasiliane: mhegera@gmail.com 0754-826272



Maoni 1 :

  1. watekaji wa Dr Stephen Ulimboka hawafahamiki walipo, mauaji ya Daud Mwangosi, usanii mtupu, mashambulizi dhidi ya Absalom Kibanda ah shauri zake, je uslama wetu upo wapi? je tutafika?

    JibuFuta